Uonevu mitandaoni si suala la mataifa yaliyoendelea tu-UNICEF

4 Septemba 2019

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa kijana mmoja kati ya 3 katika nchi 30 amesema aliwahi kuwa muathirika wa uonevu  mtandaoni huku kijana mmoja. 

Ripoti hiyo iliyotolewa leo ni ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ukatili dhidi ya watoto.

Takribani robo tatu ya vijana walioshiriki kura hiyo ya kutoa maoni bila kufichua utambulisho wao,  kupitia mbinu yenye jina U-Report, wametaja mitandao ya kijamii ikiwemo: Facebook, Instagram, Snapchat naTwitter ndiko uonevu mitandaoni unafanyika zaidi.

Akizungumiza ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore amesema, "madarasa yenye muunganiko humaanisha kuwa shule haikomi pindi mwanafunzi anapoondoka shule, halikadhalika uonevu shuleni."

 Ameongeza kwamba, “kuimarisha mazingira ya vijana ya shule ni kuhakikisha mazingira bora mtandaoni na nje ya mtandao."

Kupitia utafiti vijana waliulizwa kwa njia ya ujumbe mfupi maswali kuhusu uzoefu wao katika uonevu mtandaoni na ukatili kuhusu pale vitendo hivyo vinafanyika mara nyingi na ni nani kwa mtazamo wao ana jukumu la kumaliza vitendo hivyo ambapo utafiti unasema watu asilimia 32 ya walioshiriki utafiti wanaamini kwamba serikali ina wajibu wa kutokomeza uonevu mtandaoni na asilimia 31 wakisema walio na wajibu wa kutokomeza vitendo hivyo ni vijana na kampuni za intaneti.

Moja ya ujumbe muhimu ni kwamba ni wazi kuwa kutokana na mawazo yao kuna umuhimu wa watoto na vijana kushiriki na kushirikiana kwani kwa mujibu wa utafiti mtazamo ni kwamba jukumu liko mikononi mwa wengi.

Ripoti imesema takriban watu 170,000 walioshiriki wana  umri wa kati ya miaka 13- 24 wakitka Albania, Bangladesh, Belize, Bolivia, Brazil, Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Ecuador, Ufaransa, Gambia, Ghana, India, Indonesia, Iraq, Jamaica, Kosovo, Liberia, Malawi, Malaysia, Mali, Moldova, Montenegro, Myanmar, Nigeria, Romania, Sierra Leone, Trinidad na  Tobago, Ukraine, Vietnam na Zimbabwe.

Ripoti hiyo imesema matokeo ya utafiti yanaondoa dhana ya kwamba uonevu mtandaoni miongoni mwa wanafunzi ni suala linalojitokeza katika nchi za vipato vya juu kwa mfano asilimia 34 ya washiriki wa utafiti walio nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara wamesema wamewahi kuwa waathirika wa uonevu mtandaoni. 

Asilimia 39 walisema wanajua vikundi mtandaoni na  ndani ya jamii ya shule ambako wanafunzi hubadilishana taarifa za wanafunzi wenzano kwa minajili ya uonevu.

Ili kutokomeza uonevu na ukatili ndani na karibu na shule, UNICEF na wadau wanatoa wito wa hatua za haraka kutoka sekta zote ikiwemo kutekeleza será kwa ajili ya kulinda vijana kutoka uonevu, kuweka vituo na vifaa vya kutoa msaada kwa watoto na vijana, kuimarisha viwango na matumizi na watoa huduma za mitandao ya kijamii, kutoa mafunzo kwa walimu na wazazi kuhusu kuzuia na kukabiliana na uonevu mitandaoni na nje hususan kwa makundi yaliyo hatarini.

Kama sehemu ya kutokomeza ukatili ya UNICEF  #ENDviolence ndani na karibu na shule, watoto na vijana kutoka kote ulimwenguni walitoa andiko la vijana la #ENDviolence au tokomeza ghasia la mwaka 2018 wakitoa wito kwa vijana, walimu, wazazi na wao wneyewe katika kutokomeza ukatili na kuhakikisha kwamba wanafunzi wanajihisi salama ndani na karibu na shule ikiwemo kutoa wito kwa ulinzi mitandaoni

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud