Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchunguzi lazima ufanyike kufuatia kupasuka kwa bwawa Brazil:UN

Eneo lililoharibiwa mpasuko wa bwawa huko Brumadinho, Brazil.
Presidência da República/Divulgação
Eneo lililoharibiwa mpasuko wa bwawa huko Brumadinho, Brazil.

Uchunguzi lazima ufanyike kufuatia kupasuka kwa bwawa Brazil:UN

Amani na Usalama

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kufanyika haraka uchunguzi wa kina na huru kufuatia kupasuka kwa bwawa huko Minas Gerais nchini Brazil mnamo Januari 25 mwaka huu , hilo likiwa ni tukio la pili linalohusisha kampuni moja katika kipindi cha miaka mitatu.

 

 

Katika wito huo uliotolewa leo wataalam hao wamesema makumi ya watu walipoteza maisha na mamia wengine bado hawajulikani waliko katika zahima mgodi wa Córrego do Feijão unaomilikiwa na kampuni ya madini ya Vale. Wataalam hao wametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza Maisha na kuonyesha mshikamano wao na waathirika wa janga hilo. Wakisistiza umuhimu wa uchunguzi wataalam hao wamesema “Zahma hiyo inahitaji uwajibikaji na kuhoji hatua katika zahma hiyo ya mdogo wa Samarco miaka mitatu iliyopita wakati janga la mafuriko ya maji taka ya mgodi huo lilipokatili Maisha ya watu 19 na kuathiri wengine mamilioni karibu nae neo la Mariana.”

Wameitaka serikali kuwajibika na kufanya kila liwezekanalo katika mamlaka yake kuzuia majanga mengine kama hayo na kuwafikisha kwenye mkono wa sharia wahusika zahma hii, pia wameelezea hofu yao kuhusu juhudi za ulinzi wa jamii na mazingira nchini Brazil katika miaka ya karibuni.

Wametoa wito kwa serikali ya Brazil kutoa kipaumbele katika kutathimini masuala ya usalama kwenye mabwawa yaliyopo na kuthibitisha leseni na ukaguzi wa masuala ya usalama ili kuzuia kutokea tena kwa majanga na ajali na wameitaka serikali hiyo kutoruhusu ujenzi wa mabwa mapya au shughuli zozote ambazo zitaathiri usalama wa mabwa yaliyopo hadi pale usalama wake utakapohakikishwa.

Mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu taka za sumu Baskut Tuncak ametoa wito maalumu wa kuwepo kwa uchuhugi huru, wazi, wa haraka na kuzingatia suala la taka za sumu kwenye uchunguzi huo, na kutaka kuwepo upatikanaji wa taafifa bila vikwazo kwa umma na kutaka kuwe na hatua za tahadhari mara moja.

Na kwa upande wa kamopuni ya madini ya Vale wataalam wameitaka iwajibike kwa kubaini, kuzuia na kuzingatia haki za binadamu , pia kushirikiana kikamilifu na serikali katika kuhakikisha uchunguzi wa janga hilo.