Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Benki ya Dunia kuachia madaraka mwishoni mwa mwezi huu.

Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim ambaye ametangaza kung'atuka wadhifa huo ifikapo mwishoni mwa mwezi  huu wa Januari mwaka 2019
Benki ya Dunia
Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim ambaye ametangaza kung'atuka wadhifa huo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Januari mwaka 2019

Rais wa Benki ya Dunia kuachia madaraka mwishoni mwa mwezi huu.

Ukuaji wa Kiuchumi

Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim leo hii mjini Washington, Marekani ametangaza kuwa mwishoni mwa mwezi huu ataachia wadhifa huo alioshikilia kwa kipindi cha miaka sita.

Bwana Jim kupitia taarifa iliyotolewa na Benki hiyo amesema “imekuwa ni heshima kubwa kuhudumu kama rais wa taasisi hii inayoheshimika. Kazi ya Benki ya Dunia ni muhimu zaidi hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote kutokana na kuongezeka kwa matarajio ya watu maskini na pia kuongezeka kwa matatizo kama mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa, njaa na ongezeko la wakimbizi. Kutumikia kama rais na kuisaidia taasisi hii katikati ya changamoto hizi zote imekuwa ni fursa kubwa.”

Chini ya uongozi wa rais huyo wa 12 wa Benki ya Dunia, kwa msaada wa nchi wanachama 189, Benki ya Dunia mwaka 2012 iliweka malengo mawili, moja likiwa kumaliza ufukara ifikapo mwaka 2030 na kuboresha mafanikio ya pamoja, kwa kuzingatia asilimia 40 ya idadi ya watu katika nchi zinazoendelea. Malengo haya sasa yanaiongoza taasisi katika kazi zake za kila siku duniani kote.

Bwana Jim ambaye ana asili ya Korea Kusini amekuwa rais wa Benki ya Dunia tangu mwaka 2012.

Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia Kristalina Georgieva, atachukua mamlaka ya urais wa mpito wa benki hiyo kuanzia Februari Mosi.