Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia na Ujerumani kushirikiana zaidi katika miradi ya maendeleo barani Afrika.

Wafanyakazi wa kiwandani
World Bank/Flickr
Wafanyakazi wa kiwandani

Benki ya Dunia na Ujerumani kushirikiana zaidi katika miradi ya maendeleo barani Afrika.

Ukuaji wa Kiuchumi

Benki ya dunia na wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya Ujerumani, (BMZ) wametangaza kuimarisha ushirikiano wao kwenye miradi ya maendeleo ya kiuchumi katika nchi sita barani Afrika. 

Ujerumani  itaongeza msaada wa kifedha ili kuchagiza juhudi za watalamu wa Benki ya Dunia zinazoendelea kwa ajili kuchochea uwekezaji, upatikanaji wa ajira na mandeleo endelevu ya kiuchumi.

Ubia huu umefuatia makubaliano yaliyofikiwa  kati ya BMZ na Benki ya Dunia kwenye kongamano la uwekezaji mnamo Oktoba 30, 2018 mjini Berlin.

Nchi zitakazonufaika ni Morocco na Tunisia zilizopo Kaskazini mwa Afrika, Côte d’Ivoire, Ethiopia, Ghana, na Senegal kusini mwa jangwa la Sahara.

Nchi hizo zitapata msaada wa kifedha kuwezesha utoaji wa msaada wa kiufundi, kuboresha sera za maendeleo katika sekta zikiwemo nishati endelevu, umeme, mafunzo ya ujuzi wa kazi, sera ya uwekezaji na usimamizi wa ardhi.

Mkuu wa Benki ya Dunia Kristalina Georgieva amesema ushirikiano huu unalenga kusaidia mamilioni ya vijana watakaongia soko la ajira mbeleni.

Ameipongeza serikali ya Ujerumani kwa kukumbatia ushirikiano huu kwa wakati muafaka ambao upo kwenye ajenda ya maendeleo.