Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hawana bima ya afya- ripoti ya WHO, Benki ya dunia

Nusu ya idadi ya watu duniani bado wanakabiliwa na ukosefu wa huduma muhimu ya bima ya afya. Picha: World Bank

Nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hawana bima ya afya- ripoti ya WHO, Benki ya dunia

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema nusu ya idadi ya watu duniani hawapati huduma muhimu za afya huku wakitumia asilimia 10 ya mapatao yao kusaka huduma hizo na hivyo kutumbukia kwenye umaskini. Taarifa zaidi na Selina Jerobon.

(Taarifa ya Selina Jerobon)

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo huko Tokyo, Jaopan na shirika la afya ulimwenguni, WHO na Benki ya Dunia ikisema idadi hiyo ya watu hawana uwezo wa kumudu gharama za huduma za afya.

Nats..

Mathalani kupitia video hii.. mashirika hayo yanasema takribani watu  milioni 800 hutumia asilimia 10 ya mapato yao kusaka huduma ya afya kwa ajili yao au kwa mtoto mgonjwa au mwanafamilia.

Hali hii inawatumbukiza kwenye umaskini wa kupindukia.

Nats..

Dkt. Tedros Ghebreyesus ambaye ni mkurugenzi mkuu wa WHO amesema, ni jambo lisilokubalika kwamba nusu ya idadi ya watu duniani hawapati huduma muhimu za afya na hivyo amependekeza kuwa ni muhimu huduma ya afya ikapatikana kila pahala.

Amesema hatua hii ya afya kwa wote itawezesha watu kupata matibabu popote pale walipo duniani.

Naye Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim amesema watajitahidi kuhakikisha mahitaji muhimu ya huduma za afya zinapatikana kwa kila mtu hususan katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jngwa la Sahara.