Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yaleta ahueni kwa wakulima wa tangawizi Myanmar

Kilimo bila mafunzo juu ya kukabiliana na kemili za kilimo ni hatari kwa wakulima na walaji
UNICEF/Adrak
Kilimo bila mafunzo juu ya kukabiliana na kemili za kilimo ni hatari kwa wakulima na walaji

ILO yaleta ahueni kwa wakulima wa tangawizi Myanmar

Afya

Shirika la kazi duniani, ILO limechukua hatua kusaidia wakulima wa zao la tangawizi nchini Myanmar ambao wamekuwa wakiathirika kiafya kutokana na kilimo cha zao hilo. 

Katika jimbo la Shan nchini Myanmar barani Asia, zao la tangawizi linawakilisha njia muhimu ya maisha kwa mamia ya wakulima. 

Hata hivyo wamekuwa wakiathirika kiafya siyo tu kwa sababu ya kufanya kazi kwa saa nyingi chini ya jua kali, bali pia kemikali zinazotumika katika kilimo hicho.
 
Uba Loon mmoja wa wakulima anasema kilimo cha tangawizi kinahusisha kazi ngumu ya kulima siku nzima juani na kunyanyua mizigo mizito wakati wa kuvuna lakini hatari zaidi iko kwenye dawa za kuua wadudu.
 
“’Matumizi ya sumu za kuua wadudu ni hatari sana…”
 
Ili kupambana na hali hiyo, shirika la kazi kazi duniani ILO kupitia mradi wake wa Vision Zero Fund linawapatia wakulima taarifa na elimu ya matumizi bora ya kemikali za kilimo.

Chini ya mradi huo wakulima wa tangawizi wanafundishwa kuhusu usalama wa afya ili kupunguza hatari zinazotokana na uzalishaji wa zao hilo.
 
Mariana Infante Villarroel, mshauri mkuu katika mradi huo wa ILO nchini Mynmar anasema,

“Tunawafundisha kuhusu usalama na afya na mambo kadha kuhsu jinsi ya kudhibiti wadudu kisha mwisho wanasema mambo ambayo yanaendana na jamii yao”
 
Mkulima Ko Lwin OO baada ya mafunzo anasema,
 
“Awali sikufahamu jinsi ya kujilinda na hatari zitokanazo na kilimo na sikujali. Sasa ninafahamu jinsi ya kujipanga”