Washindi wa habari bora kuhusu uhamiaji watangazwa

18 Disemba 2017

Ikiwa leo ni siku ya wahamiaji duniani, shirika la kazi ulimwenguni ILO limetangaza washindi wanne wa shindano la kimataifa la uandishi wa habari na uandaaji vipindi chanya kuhusu uhamiaji na ajira.

Washindi hao ni miongoni mwa kazi 350 zilizowasilishwa kutoka nchi 73 duniani ambapo katika ripoti zao kwenye vyombo vya habari walionyesha jinsi wenyeji walivyowapokea vyema wahamiaji na pia walivyoweza kupata ajira na kuimarisha utangamano.

Miongoni mwa washindi ni Christopher Livesay aliyeangazia jinsi wahamiaji na wakimbizi wanakaribishwa kwenye kijiji cha Riechi nchini Italia.

Katika makala yake ya dakika 10, Christopher alitembelea kijiji hicho na kushuhudia wakimbizi na wahamiaj kutoka Somalia, Syria, Pakistan na Albania wakiishi vyema na wenyeji, na mabango kila kona ya makaribisho kwa wageni  hao.

Yasmeeni kutoka Pakistan anasema..

(Sauti ya Yasmeen) 

“Hapa ni tofauti, hakuna mtu anayetuita na kutuambia kila siku rudini kwenu. Tunafurahia kwenda shuleni na watoto wetu. Tunaweza kusema tuko huru.”

Kijiji cha Riechi kina watu 1800 ambapo kati yao 400 ni wahamiaji ambao wanafundishwa kujifunza kiitaliano ili waweze kutangamana vyema.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter