Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wanaweza kuwa na mchango chanya kwenye nchi zinazowapokea

 Kanisa ya Mtakatifu Stephen,Stephansplatz, Vienna, Austria.
UN Photo/ Rocio Franco
Kanisa ya Mtakatifu Stephen,Stephansplatz, Vienna, Austria.

Wakimbizi wanaweza kuwa na mchango chanya kwenye nchi zinazowapokea

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR linasema mji wa Vienna nchini Austria umeandaa nyumba, huduma za afya, madarasa ya lugha na programu za elimu kwa ajili ya wakimbizi na hivyo kuunga kampeni za shirika hilo za miji na manispaa zinazosaidia wakimbizi. 

Vienna mji mkuu wa Austria, wenye rekodi ndefu ya kusaidia wakimbizi baada ya vita, hii leo, jiji hilo ambalo limekua kwa sababu ya wahamiaji wa ndani na wale wa muungano wa Ulaya, lina idadi ya watu milioni 1.8.

Ujio wa maelfu ya wakimbizi katika mwaka 2015 ilikuwa ni changamoto kubwa lakini halikuwa jambo la iwapo jiji hilo linatakiwa kuwakaribisha, bali suala lilikuwa ni kwa namna gani.

Widad Alghamian, mkimbizi mwalimu kutoka Syria anasema,“Ninapenda kuwa hapa na kutembeatembea kwa sababu jiji hili lionaonekana kama mji wa zamani wa Damascus, Syria. Pia hapa kuna ushawishi wa kihistoria wa unanikumbusha jiji langu”

Familia ya Widad ni moja ya maelfu ya wakimbizi ambao wameifanya Vienna kuwa nyumbani kwao na jiji linawasaidia kwa kuwakaribisha.“Kimsingi siyo kuwa kila kitu kinafanana lakini kwa kuwa na familia yangu yote hapa, ninajisikia kuwa niko nyumbani”

Pamoja na hivi karibuni Austria kupunguza idadi ya wakimbizi inayowasaidia, jiji la Vienna linaendelea kuwasaidia wakimbizi kwa kutumia akiba yake ya fedha na pia kiasi kutoka Muungano wa Ulaya.

Halikadhalika, jiji linasaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na makundi ya wakimbizi ambao wanatafuta kujisaidia wenyewe.

Jürgen Czernohorszky, Meya wa jiji la Vienna anasema,“Kama jiji, huwezi kuongoza mjadala kwa kufumba macho na kusema, ‘siwataki wawe pale’. Wako hapa na unatakiwa kufanya jambo-waweze kujifunza lugha, kuwawezesha kujimudu wao wenyewe na kupata mafanikio yao na kushiriki katika huumchezo unaoitwa jamii”

Tayari mradi wa CORE unaondeshwa na shirika la kiraia unawapatia wakimbizi fursa za kutekeleza mawazo yao, mathalani Widad alitaka kuwa mwalimu hivyo kimempatia chumba ili aweze kurejelea kazi yake ya ualimu aliyokuwa akifanya Damascus, akifundisha lugha ya kiarabu kwa watoto wakimbizi. 

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.