Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzingatia wa sheria na ushirikiano vimependezesha mji wa Kigali:Meya

Moja ya mitaa ya mji mkuu wa Rwanda, Kigali
UN /Rick Bajornas
Moja ya mitaa ya mji mkuu wa Rwanda, Kigali

Uzingatia wa sheria na ushirikiano vimependezesha mji wa Kigali:Meya

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kigali ambao ni mji mkuu wa Rwanda barani Afrika unatajwa kuwa na usafi wa hali ya juu!

Sera za serikali, ushirikiano baina ya wadau wote na serikali na pia utekelezaji wa sheria vimechangia kwa kiasi kikubwa mji wa Kigali nchini Rwanda kuwa mzuri, wenye mnepo na endelevu katika mazingira.

Hayo ni kwa mujibu wa meya wa jiji la Kigali Marie-Chantal Rwakazina , ambaye katika siku hii ya miji duniani amemueleza Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili siri ya mafanikio ya mji huo.

Hatua hizo za mji wa Kigali zinakuja wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasisitiza miji iwe makini kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya wakazi ambao kila uchao wanahamia maeneo hayo kwa matarajio ya kuwa na maisha bora zaidi.