Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Komesheni ukatili dhidi ya watoto Yemen:UNICEF

Suad, mwenye umri wa miaka 18, akiwa katikati mwa barabara itoakyo Sana'a, mji mkuu wa yemen na saada akiwa na mpwa wake mwenye umri wa miaka minne.
Giles Clarke/OCHA
Suad, mwenye umri wa miaka 18, akiwa katikati mwa barabara itoakyo Sana'a, mji mkuu wa yemen na saada akiwa na mpwa wake mwenye umri wa miaka minne.

Komesheni ukatili dhidi ya watoto Yemen:UNICEF

Amani na Usalama

Ukatili dhidi ya watoto ni lazima ukomeshwe mara moja, hakuna visingizio tena. Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Geert Cappelaere ametoa wito huo kufuatia shambulizo la anga lililotokea leo nchini Yemen na kukatili maisha ya watoto wengi na wengine kujeruhiwa katika mjini wa Sa’ada Kaskazini mwa Yemen.

Cappelaerre amesema shambulio hilo dhidi ya basi lililokuwa na wanafunzi ni la kusikitisha na kuhuzunisha , na watoto wote hao wamearifiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 15 huku duru zikisema makumi ya watoto wameuawa katika shambulio hizo.

Akisistiza umuhimu wa kukomesha ukatili dhidi ya watoto amehoji “kweli dunia inataka kupotea zaidi kwa maisha ya watoto wasio na hatia ndio wakomeshe vita hivi vya kikatili dhidi ya watoto Yemen”?

Amezitaka pande zote kinzani katika mzozo wa Yemen kuheshimu haki za kimataifa za binadamu zikiwemo za watoto.