Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pakistan acheni sheria zinazoibagua jamii ya Ahmadiyya :UN

Mchungaji akiwa katika maeneo ya milimani sehemu za Himalaya kaskazini mwa Pakistan.Uchaguzi mkuu umefanyika nchini kote pamoja na maeneo hayo.
IFAD/Joanne Levitan
Mchungaji akiwa katika maeneo ya milimani sehemu za Himalaya kaskazini mwa Pakistan.Uchaguzi mkuu umefanyika nchini kote pamoja na maeneo hayo.

Pakistan acheni sheria zinazoibagua jamii ya Ahmadiyya :UN

Haki za binadamu

Wataalam  wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka  serikali ya Pakistan kufuta vipengele vya sheria yake ya uchaguzi vinavyosababisha kuteswa na kulengwa na mashambulizi jamii ya Ahmadiyya kunapozuka vurugu nchini humo.

Wataalam hao wameonyesha wasiwasi kufuatia  uchaguzi uliofanyika hii leo wakisema, mfumo wa sasa washeria ya  uchaguzi unataka , “Jamii ya Ahmadiyya ambayo kujitangaza kuwa sio waislamu ili waweze kuorodheshwa na kupiga kura”.

Wameongeza kwa sheria hiyo inaweza kuwa na athari kubwa kwa kiwango cha ushiriki wa jamii ya Ahmadiyya katika mchakato wa kisiasa.

Ingawa jamii ya Ahmadiyya inajitambulisha kama Waislamu, marekebisho ya Katiba ya Pakistan ya mwaka 1974 yalitangaza jamii hiyo kama sio Waislam. Na hali hiyo bado haijabadilishwa  katika Katiba ya sasa, hali ambayo wataalam hao wanasema  inaendelea kukiuka haki zao za  kiraia, za kisiasa, za kiuchumi, za kijamii na za kitamaduni kwa sababu ya tofauti ya dini yao ikilinganishwa na watu wengine walio wengi katika jamii.

Aidha, Ofisi ya haki za binadamu inasisiza  kuwa haki ya kukiri na kufuata dini au Imani fulani ni ya mtu binafsi na haipaswi kuingiliwa, kwa mujibu wa kifungu cha pili cha Azimio la Umoja wa Mataifa la 1992 kuhusu haki za watu kutoka, taifa au Kikabila, Kidini na Lugha za jamii ndogo ndogo.

Ofisi hiyo pia imetoa wito kwa serikali ya Pakistan kuondoa adhabu ya kifo kwa makosa ya kukufuru, kukashifu au kulaani masharti hayo kuwa hayaendani na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu. 

Wataalam hao pia wamewasiliana na Serikali ya Pakistani ili kupata ufafanuzi kuhusu sheria na masuala mengine yanayozua wasiwasi.