Chondechonde wapokeeni wahamiaji waliokwama melini Mediterranea UNHCR

11 Juni 2018

Shirika la kuwahudumia wakimbizi duniani UNHCR limeziomba serikali husika  kuwakubalia mamia ya watu ambao wamekwama katika bahari ya Mediterani wakiwa ndani ya meli ya  the Aquarius kuingia nchini mwao.

Wito huo umetolewa jumatatu na mjumbe maalum wa UNHCR katika eneo la Mediterani ya kati,Vicent Cochetel, ikiwa leo ni siku ya pili tangu watu hao wakiwa baharini ndani ya meli baada ya kuokolewa  jumammosi.
 
Anasema watu hao wanakabiliwa na changamoto nyingi na wanahitaji msaada wa haraka kwani vitu walivyokuwa navyo kama chakula na maji vinapungua na suala la nani achukue dhamana na vipi mataifa yagawane jukumu hilo yatafuata baadae baada ya watu hawa kuondolewa kutoka majini.

Takriban watu 629 wako ndani ya meli hiyo ya Aquarius, kati yao kuna watoto ni zaidi ya 100. Meli hiyo iko   katika eneo kati ya Malta na Italia na hadi sasa hakuna nchi iliyokubali  na kuruhusu meli hiyo kutia nanga katika bandari yake ili watu hao waweze kushuka.

Italy mwaka huu 2018 imeshapokea takriban wahamiaji 13,706, hii ikiwa ni idadi ndogo ikilinganishwa na miaka iliyotangulia.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter