Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri heshimuni haki za mahabusu-UN

Wakosoaji serikali kupitia mitandao ya kijamii mbaroni Misri
UNICEF
Wakosoaji serikali kupitia mitandao ya kijamii mbaroni Misri

Misri heshimuni haki za mahabusu-UN

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka serikali ya Misri kuwaachilia huru mara moja wale wote wanaoshikiliwa kwa sababu za kutekeleza haki za zao za kibinadamu.

Mwito huo umetolewa leo mjini Geneva Uswisi katika taarifa iliyotolewa  na msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani.

Msemaji amesema kuwa kampeini mpya ya kuwakamata , kuwahoji na kuwaweka ndani wanaharakati, wana blogi na waandishi habari katika kipindi cha  wiki chache zilizopita, yaonyesha kama ishara ya kuongezeka kwa kamatakamata dhidi ya haki uhuru wa kujieleza, kukutana na kujumuika nchini humo.

waachilieni mara moja wanaharakati

Taarifa inasema kuwa baadhi ya waliokamatwa mwezi Mei ni bloga mashuhuri nchini humo Wael Abbas, wakili na mwanaharakati Haytham Mohamadein ambao wametuhumiwa  kuitisha maandamano haramu huku mwengine alikamatwa kwa kutuma ujumbe wa Twitter akikosoa  mpango wa rais wa kuigawia Saudi Arabia visiwa viwili katika baharí ya Sham.

Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ameongeza waliokamatwa hawakupewa waranta kwanza kuwa na kesi zinazowakabili hukumu zake ni vifungo gerezani vya muda mrefu.Ametoa mfano wa mwandishi habari Ismail Alexandria  ambae amekuwa korokoroni tangu Novemba ya mwaka wa 2015, Mei 22 mwaka huu alihukumiwa  na mahakama ya kijeshi kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kuwa mwanachama wa kundi haramu na pia kusambaza taarifa za uongo.

Jiji la Cairo Misri
Dominic Chavez/World Bank
Jiji la Cairo Misri

Kamatakamata mpya ilichochewa na hatua ya tamko la mwezi febuari la mwendesha mashataka mkuu  aliwaamuru wendesha mashakata kuchunguza  mitandao ya kijamii aliyosema kuwa eti inasambaza uongo na habari zisizo za ukweli.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa ndio ikataka serikali ya Misri, mara moja kuwachilia huru wale wote ambao wanashikiliwa kwa  sasa  kutokana na hatua yao ya kutekeleza haki zao za kimsingi.