Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahanga na watetezi wa haki za binadamu wanaadhibiwa vikali:UN

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour. Picha: MINUSCA

Wahanga na watetezi wa haki za binadamu wanaadhibiwa vikali:UN

Haki za binadamu

Watu kote duniani wanakabiliwa na adhabu na vitisho vikubwa kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika masuala ya kupigania haki za binadamu, jambo ambalo ni “aibu kubwa” imeonya leo ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti hiyo inasema kuna ongezeko la wigo wa kutisha na athari za kuadhibiwa kwa waathirika, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu.

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambayo mwaka huu ni ya tisa na ya aina yake, inatanabaisha jinsi waathirika, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kote duniani wanavyokumbana na mtihani mkubwa na mateso, ikionya kwamba mwenendo huu unawakatatisha tamaa wengine wasishirikiane na Umoja wa Mataifa na kuwfanya wajiulize mra mbili kwanza kabla ya kutoa ushirikiano.

Taarifa zilizoainishwa katika ripota ni za nchi kwa nchi na zimegawanywa katika mafungu mawili  zikijumuisha madai ya mauaji, mateso na unyanyasaji, kukamatwa kiholela na kuswekwa kizuizini, kufuatiliwa, uhalifu, na kampeni za unyanyasaji wa umma zinazowalenga waathirika na watetezi wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa ripoti visa hivyo vimeorodheshwa katika nchi 38 ambapo baadhi ni wanachama wa sasa wa baraza la haki za binadamu nazingine zimekuwa zikitajwa katika ripoti hiyo kila kwamba tangu ilipozinduliwa mwaka 2010.

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya haki za binadamu Andrew Gilmour amesema yaliyoorodheshwa katika ripoti ni sehemu tu,wakati mengi zaidi huripotiwa katika ofisi ya haki za binadamu. Akiongeza kuwa “tunashuhudia ongezeko la vikwazo vya kisiasa, kisheria na kiutawala vikitumika kuitisha na kuinyamazisha jamii, huku sheria kali zilizopo na baadhi ya mpya zinatumika kuwabana wanaotoa ushirikiano kwa Umoja wa Mataifa.”

 Nchi 29 zimetajwa kuwa na visa vipya zikiwemo Rwanda, Sudan Kusiki, Mali, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Gilmour aliye na kibarua cha kulishughulikia uala hilo atawasilisha ripoti yake kwenye Baraza la Haki za binadamu Septemba 19.