Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ocha yaridhishwa na matumizi mazuri ya misaada ya kibinadamu

Wanawake huko Ganyiel jimbo la Unity nchini Sudan Kusini wakisubiri mgao wa chakula. Hali ni mbaya ya chakula.
OCHA/Gemma Connell
Wanawake huko Ganyiel jimbo la Unity nchini Sudan Kusini wakisubiri mgao wa chakula. Hali ni mbaya ya chakula.

Ocha yaridhishwa na matumizi mazuri ya misaada ya kibinadamu

Msaada wa Kibinadamu

Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, imebaini utelekezaji  mzuri  wa misaada ya kibinadamu  kwa kuzingatia muda na mahitaji ya waathirika kwa baadhi ya nchi zilizonufaika na mfuko wa misaada wa CBPFs .

OCHA kupitia   mfuko huo mfuko unaopokea fedha kwa wahisani na kuziratibu kwa nchi husika , ilipokea  kiasi cha dola milioni 835 zilitolewa na nchi 26, na wahisani binafsi ili  kusaidia  miradi 1,256  katika nchi 18 duniani kupitia  miradi mbalimbali kama afya, chakula, maji safi na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Ripoti ya OCHA imetaja nchi zilizonufaika kuwa ni pamoja na Afghanistan, Jamuhri ya Afrika ya kati CAR, Colombia, DR Kongo,Ethiopia, Iraq,Lebanon.,Myanmar na Nigeria.

Ripoti hiyo imebaini kuwa fedha hizo zimefanya kazi  kama ilivyokusudiwa na wahisani kwa kuzingatia uwazi, muda na maeneo husika ya vijijini na kwa walengwa ambao ni wathirika wa migogoro ya kivita na majanga mbalimbali ya kibinadamu.

James Keah Nirew ambaye anaongonza moja ya mashirika yalionufaika na msaada huu, amesema wao kama shirika linalohudumia jamii ya vijijini, kupewa  nafasi katika maamuzi ya sekta ipi na eneo lipi  fedha zitumike  ni jambo jema katika utekelezaji na katika kutoa kipaumbele katika misaada ya kibinadamu kwa waathirika.

Katika mgawanyo  wa fedha hizo, mashirika ya kimataifa yalipokea kiasi cha dola milioni 295, yakifuatiwa na mashirika ya Umoja wa mataifa yaliyopokea dola   milioni 205,  mashirika ya kitaifa dola milioni 144 na mwisho mashirika ya msalaba mwekundu na hilali nyekundu yaliyopokea dola milioni 6.