Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa umri wangu ni miaka 17 tu lazima niwalee wadogo zangu.

Mtoto  akiwa nje ya nyumba katika kambi ya wakimbizi Bangladesh
Picha ya UNICEF/Nybo
Mtoto akiwa nje ya nyumba katika kambi ya wakimbizi Bangladesh

Ingawa umri wangu ni miaka 17 tu lazima niwalee wadogo zangu.

Wahamiaji na Wakimbizi

Baada ya kuuliwa kwa wazazi wake na watu wenye silaha msichana mwenye umri wa miaka 17 alichukuwa jukumu la kuwalewa wadogo za watatu kutoka Myanmar hadi Kutupalong nchini Bangladesh

 

Huyo ni Mabia , Binti wa miaka 17,mkimbizi wa Kirohingya aliyefanikiwa kukimbia machafuko ya kikabila kutoka Kaskazini mwa Myanmar hadi bangladesh akiwa na yeyé  tu na wadogo zake watatu .

Akiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kutupulong, Mabia anasema alichukua jukumu la kutafuta hifadhi nchini Bangladesh kukimbia machafuko nchini mwao, ambapo yeyé ndugu zake watatu wenye umri wa miaka 16 mwingine 15 na mdogo wao wa mwisho 15, walitembea umbali mrefu na baadae kufika mpakani na kupokelewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja ya vikosi vya usalama nchini Bangladesh.

Kkiongea Kwa uchungu mkubwa ,Mabia ambaye kwa sasa yupo katika kituo cha watoto yatima na watoto wengine 5,600 ambao wazazi wao walipotea au kuuawa , anasema ,”ana majukuma yakuilinda familia , anatamani afe tu kwani majukumu ya kuwahudumia wadogo zake yamemzidi sana”.

Licha ya majukumu ya kutafuta malazi, chakula na mahitaji mengeni ya kujikimu, Binti huyo mdogo anatakiwa kuhakikisha wadogo zake wanapata matibabu ya afya kama ilivyo taratibu za mashirika ya kibinadamu kwa wakimbi.

Ingawa ni changamoto kubwa sana kwake , Mabia anasema , atahakikisha anawalea wadogo zake kwani hataki wakumbuke mambo mabay waliopitia.