Tekinolojia ya habari na mawasiliano yafufua matumaini ya wakimbizi Ujerumani

Wanafunzi wa chuo cha habari ya mawasiliano, ReDI Ujerumani  wakiwa darasani.
Picha ya UNHCR/Gordon Welters
Wanafunzi wa chuo cha habari ya mawasiliano, ReDI Ujerumani wakiwa darasani.

Tekinolojia ya habari na mawasiliano yafufua matumaini ya wakimbizi Ujerumani

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Hatua ya kutoa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano au TEKNOHAMA kwa wakimbizi kupitia shule ya ReDi nchini Ujerumani, imefufua matumaini ya mustakhbali wao  waliokuwa wameukatia tamaa.

Nats................

Huyo ni Bi Rita Butman ambaye kwa sasa anafanya kazi ya kujitolea katika chuo cha ReDI. Akisema shule ya ReDi imebadili maisha yake,kwani  alikuwa akifanya kazi ya kuosha vyombo lakini sasa , ameajiriwa  na kampuni ya SISCO ambayo ni moja ya makampuni makubwa ya mawasiliano dunaini. Rita ni moja  kati ya wakimbizi wa kwanza  waliopata fursa ya kusoma katika chuo cha ReDi kinachotoa mafunzo ya tekinolojia ya mawasiliano kwa  wakimbizi wanawake ili kuwajengea uwezo na kuwapa fursa za kupata ajira nzuri nchini Ujerumani.

Chuoni hapo hakubahatika peke yake, Anan Jakich mkimbizi kutoka Syria ni mmoja ya wanafunzi wapya   chuoni hapo hakuficha hisia zake jinsi mafunzo hao yalivyobadili mwelekeo wa maisha yake.

(Sauti ya Anan Jakich)

Nasi tungependa kuwa sehemu ya jamii hii mpya  iliyotupokea.. Sitaki kukaa tu nyumbani bila shughuli, badala yake napenda kufanya kitu cha kimaendeleo na  kuwa na mtazamo wenye tija.

Mkurugenzi wa chuo cha ReDI, Edlira Kasak, amesema programu hiyo mpya ya kidijitali ipo katika hatua ya mwanzo, kwani huu ni  mwaka wa kwanza,  na inawajumuisha wanafunzi 80 wakiwa katika makundi mawili, kwanza wanajifunza msingi wa mafunzo ya kidijitali na pili ni  la wataalamu wa tekinolojia ya mawasiliano kama alipofikia  Anan.

(Sauti Edlira Kasak)

Nadhani changamoto za wakimbi Ulaya ni fursa kwetu pia kuweza kukutana nao na kijufunza mambo mengi ambayo wanakuja nao. Watu hawa ni mustakabali bora kwa nchi walikotoka , na pia ni fursa ya kujaza zaidi ya ajira 50,000 za tekinolojia ya habari na mawasiliano hapa Ulaya na kusaidia uchumi wetu.