Dunia tuliyonayo ni moja tu hakuna haja ya kuiharibu-Guterres
Sisi binadamu hatuna rukhsa ya kuangamiza hii dunia moja tuliyo nayo, ama kukubali tofauti zetu kusababisa mateso na maumivu ambayo yanatuzuia kufaidika na manufaa ya ustaarabu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akihutubia wandishi habari mjini Backara Sweden bada ya kuwasili ambako yeyé na wajumbe wa baraza la usalama watakuwa na kikao maalum cha faragha katika nyumba ya Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld. Akisistiza kuhusu ustaarabu Guterres amesema
(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)
‘’Na ninaposhuhudia yanayoendelea leo , tunapoona migawanyiko mingi, tofauti za zamani zikirejea, migawanyiko mipya ikiongezeka mara dufu, migogoro ambayo inasababisha mateso makubwa duniani kote, na Syria ikiwa ndio mfano wa yote, ni muhimu kukumbuka maneno ya Dag Hammarskjöld.’’
Ameongeza kuwa Dag Hammarskjöld leo anabaki kama nembo madhubuti na mfano muhimu kwao kuweza kufanya mambo ambayo ni sawa, ilikuweza kuepuka utata na tofauti pamoja na kuelewa kwamba binadamu wote ni sharti kufanya kila liwezekanalo kuwa na dunia moja yenye utangamano.
Pia Katibu Mkuu pia amegusia Korea Kaskazini kuhusu uamuzi wake wa kusimamisha kwa muda majaribio yake ya nyuklia pamoja na urushaji wa makombora ya masafa marefu akisema
(SAUTI YA GUTERRES)
“ Ninaimani Korea Kaskazini, mlango baado uko wazi wa nia ya amani wa kuondoa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea.”
Pia amekariri azma ya uungwaji mkono wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kutanzua mgogoro huo tena kwa njia za amani.