Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 60 ya kifo cha Dag Hammarskjöld

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Marchi 1960.
UN Photo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Marchi 1960.

Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 60 ya kifo cha Dag Hammarskjöld

Masuala ya UM

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Septemba 09, 2021 limefanya hafla ya kumbukumbu yakuadhimisha miaka 60 ya kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.

Katibu Muu wa Umoja wa Mataifa wa sasa António Guterres, ameshiriki katika hafla hiyo na kueleza “katika kifo cha Dag, ulimwengu ulikuwa umepoteza "mtumishi mtukufu wa amani, na Umoja wa Mataifa ulimpoteza mmoja wa wakubwa wetu. ”

Hayati Hammarskjöld aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1953, akiwa na umri wa miaka 47 tu, na mpaka sasa ndio mtu mwenye umri mdogo kabisa kuwahi kushika wadhifa huo wa juu katika Umoja wa Mataifa. 

Tarehe 18 Septemba 1961, wakati wa muhula wake wa pili, alikufa kwa ajali ya ndege wakati alipokuwa njiani kwenda kujadili usitishaji vita nchini Congo.

Maadhimisho maalum yaliyofanyika mwaka huu yalilenga kutambua mafanikio ya hayati Hammarskjöld, ikiwa ishara ya kumshukuru kwa kujitolea maisha yake kutumikia umma wa ulimwengu, na kutafakari juu ya urithi wake wa kudumu aliouacha duniani kupitia kazi zake.

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa - Hayati Dag Hammarskjöld
UN Photo/MB
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa - Hayati Dag Hammarskjöld

 Mtu wa vitendo 

Akizungumzia uwezo wake wa Kazi Guterres amesema "Alikuwa mtu wa vitendo zaidi na mwanadiplomasia mahiri; alikuwa mtu wa utamaduni mkubwa, mwenye akili nzuri na uwezo wa kujadili vitu kiunyeti. Na ilikuwa shauku hii ya kina na uweledi wake mpaka kwenye masuala ya kiutamaduni ambayo ilisaidia kumfanya awe mwanadiplomasia anayeongoza wa kizazi chake."

Akikumbuka uwezo wa hayati Hammarskjöld kuzungumza karibu lugha sita, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema  "labda anajua sana lugha ya ubinadamu wetu wa kawaida – alikuwa akitambua kuna utajiri kwenye utofauti wetu, kukuza mazungumzo, kuvumiliana, na kuelewana."

Ameongeza kuwa mwanadiplomasia huyo wa raia wa Sweden alikuwa ametetea maoni kadhaa muhimu ya umoja wa Mataifa ambayo yameendelea kuheshimiwa muda mrefu hata baada kifo chake, kama vile kuweka haki za binadamu katika kitovu na na kujielekeza katika kuzilinda, "wanabaki kuwa ndio taa zinazoongoza Umoja wa Mataifa kweney ukweli wa Kaskazini.”