Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia mpya imnufaishe binadamu -IMF

Makao makuu ya shirika la fedha duniani la IMF  mjini Washington, DC Marekani
Picha ya IMF/Henrik Gschwindt de Gyor
Makao makuu ya shirika la fedha duniani la IMF mjini Washington, DC Marekani

Teknolojia mpya imnufaishe binadamu -IMF

Ukuaji wa Kiuchumi

Mwanadamu anaonekana yuko hatarini  kutokana na teknolojia ya kisasa hususan jinsi ilivyoshuhudiwa hivi karibuni ambapo data zilitumiwa kwa njia inayofanya mtu ajihisi si vizuri.Siraj Kalyango  na taarifa zaidi

Mwanadamu anaonekana yuko hatarini  kutokana na teknolojia ya kisasa hususan jinsi ilivyoshuhudiwa hivi karibuni ambapo data zilitumiwa kwa njia inayofanya mtu ajihisi si vizuri.Siraj Kalyango na taarifa zaidi

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Hayo yametamkwa katika mjadala wa mustakhbali wa kazi katika zama za sasa za maendeleo ya mawasiliano yaliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha duniani, IMF Christine Lagarde,mjini Washington Marekani.

Lagarde na viongozi wengine wakuu wa nyanja za kibiashara na teknolojia wamejadili  fursa zilizopo pamoja na changamoto za siku za usoni katika zama za sasa za maendeleo ya mawasiliano.

 
(Sauti ya Christine Lagarde)
 
“ Kampuni kadhaa kubwa za intaneti  zinadhibiti kwa kiasi kikubwa mtiririko wa data na habari, hivyo waanzilishi wa kampuni hizo ni miongoni mwa matajiri wakubwa duniani.”
 
Mkuu huyo wa IMF aliwatupia swali wanajopo wenzake ikiwa hii ni ishara kuwa historia inajirudia ambapo katika hatua iliyoonekana kama ya kutoa jibu la swali la Bi Lagarde mwanajopo mwingine , Bridget van Kralingeni kutoka kampuni tanzu ya IBM ameonya kuwa teknolojia inaweza kutumiwa kwa uzuri na ubaya.

(Sauti ya Bridget van Kralingeni)

“Data kwa upande mmoja ni tukio moja muhimu kwa wakati wetu na kwa upande mwingine ni hoja kwa huu. Majuzi tumeshuhudia data  zikitumiwa kwa  njia za kifichoficho ambazo zinamuacha mtu  akishangaa na kutaka isirudiwe tena. Hata hivyo huo ndio upande mmoja wa teknolojia. Teknoljia hizo zilizoko kwa sasa, kwa upande wa pili, zinaweza kutumiwa  sio tu kwa manufaa ya mwanadamu  lakini pia na  uzalishaji."


Wanajopo wameendelea katika mjadala wao kwa kugusia   mikakati ya ushindani ya kukuza ubunifu wakati huo huo ikijaribu kuepusha kuiletea hasara jamii.

Naye mshauri mkuu wa zamani wa ubunifu katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Alec Ross amesema kuwa data ndio malighafi ya wakati huu wa  enzi ya teknolojia ya mawasiliano na habari.