Viwango vipya vya kudhibiti wadudu wa mimea vyapitishwa: FAO

18 Aprili 2018

Mkataba wa kimataifa wa kulinda mimea IPPC leo umeidhinisha viwango vipya venye lengo la kuzuia wadudu waharibifu katika kilimo na mazingira kuvuka mpaka na kusambaa kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO viwango hivyo vilivyopitishwa ni pamoja na tiba ya kutumia viwango mbalimbali vya joto kutibu wadudu katika kilimo ikijumuisha kuwagandisha na kuwaua wadudu hao, pili viwango vya usafi katika kufunga bidhaa za mbao, na tatu kupanua wigo wa matumizi ya mvuke wa joto kuua wadudu wanaoshambulia matunda

Viwango hivyo vinabainisha mikakati na mbinu mbalimbali zinazotumika kuzuia kuzuka na kusambaa kwa magonjwa ya mimea na wadudu kwenye mazingira mapya, ili kuepuka athari zake ambazo ni kubwa kwa bayoanuai, uhakika wa chakula na biashara.

Naibu mkurugenzi mkuu wa FAO Maria Helena Semedo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka huu wa IPPC ambao hufanyika kila mwaka mjini Roma Italia amesema,  hii ni kazi yenye changamoto na jukumu kubwa, kila mwaka inakadiriwa kuwa asilimia 10 hadi 16 ya mavuno duniani hupotea kutokana na wadudu waharibifu wa mimea na kusababisha hasara ya dola bilioni 220.

Takwimu za FAO zinaonyesha kuwa bidhaa za kilimo za dola trilioni 1.1 hufanyiwa biashara ya kimataifa kila mwaka, huku chakula kikichukua  zaidi ya asilimia 80 ya jumla hiyo.Baadhi ya abiria ni watalii, na wanaelekea sehemu mbalimbali ya utalii...

Nats...

Tunapofika baharini tunashuhudia watoto wakicheza katika eneo la pwani, huku watalii wakiendelea na shughuli zao baharini...

Bwana Noor Hassan anafunguka....

"Ningependa kuhimiza watu kote ulimwenguni, ikiwa una hamu ya kuja Somalia, jisikie na ujiamini, kisha ujiunge nasi. Tunakualika Somalia, tunakualika Kismaayo, tunakualika Mogadishu, tunakualika Hargeisa, tunakualika uone Bossaso, Garowe, Belet Weyne na miji mingine mikubwa"

Na kweli tunaona ndege zikitua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Abdulleh mjini Mogadishu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter