Ganda la nanasi linaweza kubadili maisha yako-FAO

20 Aprili 2018

Ganda la nanasi nalo ni miongoni mwa mambo ambayo yakizingatiwa yanaweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

 

Je wafahamu kuwa mabaki au uchafu unaopatikana duniani vinaweza kuondoa watu kwenye umaskini na hata njaa?

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limetolea mfano wa maganda ya matunda aina ya nanasi likisema kuwa yanaweza kutumika kutengeneza vifungashio vya bidhaa ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

FAO imesema hay oleo huko Berlin nchini Ujerumani wakati wa mkutano kuhusu uchumi wa dunia unaotumia mabaki au takataka katika kuzalisha nishati au hata bidhaa.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO Maria Helena Semedo akizungumza kwenye mkutano huo amesema ugunduzi kwenye sekta ya matumizi ya takataka na mabaki hata samadi, ukichanganywa na ujuzi wa kiasili vinaweza kutokomeza njaa, umaskini na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

 Hata hivyo ameonya kuwa ni lazima kuwa makini kwa sababu si kila bidhaa itengenezwa kutokana na takataka au mabaki ni nzuri kwa tabianchi.

Badala yake amesema inategemea jinsi inavyotengenezwa hususan nishati inayotumika kuichakata.

Kwa mantiki hiyo Naibu Mkuu huyo wa FAO ametaka uratibu wa suala hilo kuanzia ngazi ya kijamii hadi kimataifa ili kuhakikisha inaleta tija na si shida.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter