Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wakaribisha maendeleo kuelekea uundaji wa eneo lisilo na silaha za nyuklia, Mashariki ya Kati

Sanamu iliyopatiwa jina "Wema washinda ubaya" iliyopo makao makuu ya UN New  York, Marekani ikiwa na sanamu ya George akichoma mkuki zimwi lililotengenezwa kwa mabaki ya silaha za nyuklia.
UN Photo/Rick Bajornas)

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amekaribisha kufanikiwa kwa Mkutano wa Uanzishwaji wa eneo huru la silaha za nyuklia na silaha zingine za maangamizi mkubwa katika Mashariki ya Kati, uliofanyika wiki hii katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

Kulingana na waandishi wa habari, katika tamko la kisiasa, Mataifa yaliyoshiriki katika Mkutano huo yangefanya kutekeleza "kwa wazi na kwa umoja" ufafanuzi wa makubaliano kwenye eneo huru la silaha za maangamizi katika Mashariki ya Kati "kwa msingi ya mipango iliyofikiwa kwa uhuru na makubaliano na Mataifa ya mkoa."

Aidha kwa mujibu wa taarifa, Mkutano ulialika mataifa yote katika ukanda ili kuunga mkono tamko la kisiasa lililopitishwa na Mkutano na kujiunga na mchakato.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Jumatatu iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikumbushia kuwa, "dunia ina maeneo matano yasiyokuwa na nyuklia huko Amerika ya Kusini na Karibea, Afrika, Asia ya Kati na Asia. Mashariki ya Kusini na Pasifiki Kusini", na kwamba hizi "pia huleta faida dhahiri za usalama na kutoa uhakikisho kwa nchi wanachama dhidi ya utumiaji au vitisho vya matumizi ya silaha za nyuklia ".