Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yapongeza kuanza kutekelezwa mkataba mpya wa kupinga nyuklia TPNW

Takribani saa sita mchana ya tarehe 9 Agosti 1945, bomu la nyuklia liliangushwa na Marekani kwenye mji wa Nagasaki na wingu zito lilienea mjini humo, picha hii ilipigwa  umbali wa kilometa 3 kutoka kitovu cha bomu hilo.
UN /Nagasaki International

Amani na Usalama

Mkataba wa kwanza wa kimataifa kwa zaidi ya miongo miwili kupinga silaha za nyuklia umeanza kutekelezwa leo na kupongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameiita hatua hiyo kuwa ni muhimu kuelekea dunia huru bila silaha za nyunklia.

Antonio Guterres amesema "Mkataba huo wa kukataza silaha za nyuklia TPNW pia kwa ujumla unawasilisha ushirika na uungaji mkono mkubwa kwa mtazamo wa kimataifa dhidi ya silaha za nyuklia".

Manusura wa nyuklia wanasemaje

Katika ujumbe wake wa video Katibu Mkuu ameyapongeza mataifa ambayo yameridhia mkataba huo na kukaribisha jukumu muhimu la asasi za kiraia katika kusongesha mbele majadiliano kuhudsu TPNW na kuanza kwa utekelezaji wake.

Mtambo wa nyuklia ulioko Busher nchini Iran.
IAEA/Paolo Contri
Mtambo wa nyuklia ulioko Busher nchini Iran.

Ameongeza kuwa "Manusura wa milipuko ya nyuk;lia na majaribio ya nyuklia wameelezea madhila na machungu makubwa ambayo yamekuwa msukumo wa dhamira za kuwepo kwa mkataba huu. Na kuanza kutekelezwa ni ushahidi tosha wa uchagizaji wao kutokana na waliyopitia."

Bwana Guterres amesema anatarajia kwa hamu kutoa muongozo kwa hatua za Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa mkataba huo, ikiwemo maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa nchi zilizotia saini mkataba huo.