Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki kufikisha ujumbe wa madhila ya uhamiaji kwa vijana:IOM

Picha kutoka video mpya toka kundi la Degg Force 3 kibao kikipatiwa jina la Falé kikieleza uhalisia wa safari ya vijana wawili kuvuka jangwa kusaka hali bora Ulaya.
IOM/Guinea
Picha kutoka video mpya toka kundi la Degg Force 3 kibao kikipatiwa jina la Falé kikieleza uhalisia wa safari ya vijana wawili kuvuka jangwa kusaka hali bora Ulaya.

Muziki kufikisha ujumbe wa madhila ya uhamiaji kwa vijana:IOM

Wahamiaji na Wakimbizi

Vijana sasa wameamua kutumia muziki wa kufokafoka au rap ili kuelezea madhila ya kuvuka jangwa la Sahara na kwenda kusaka maisha bora barani Ulaya.

Muziki wa kisasa ni nyenzo muhimu ya kufikisha ujumbe wa hatari na madhila ya uhamiaji kwa vijana wa Agfrika ya Magharibi.  Siraj Kalyango na taarifa kamili

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM ambalo linasema idadi kubwa ya vijana wa Afrika Magharibi ambao hawajaorodheshwa wanakuwa hatarini wanapojaribu kwenda kusaka mustakhbali bora ughaibuni kupitia safari za jangwani hadi Afrika Kaskazini na bahari ya Mediterranea kuingia Ulaya.

Sasa IOM, imeamua kuingia ubia na wasanii wa muziki wa Afrika Maghjaribi ili kuelimisha vijana kuhusu hatari ya kuwa wahamiaji wa kiholela na kuwashawishi kusaka mustakhbali bora karibu na nyumbani.

Mwishoni mwa wiki zaidi ya vijana 10,000 nchini Guinea walikusanyika mjini Mamou, kwa ajili ya uzinduzi video mpya ya kundi la muziki wa kufokafoka au Rap la Degg J Force 3  iliyobeba kibao  Falé  kilichoimbwa kwa lugha ya susu kikimaanisha” hadhithi ya kweli ya kusisimua ya safari ya wavulana wawili jangwani”

Video hiyo iliyofadhiliwa na mradi wa pamoja wa IOM na Muungano wa Ulaya kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji  inaelezea machungu wanayopitia maelfu ya vijana wahamiaji wanaovuka jangwa kila mwaka kwenda kusakama maisha bora kwa ajili yao na familia zao.

Mwaka 2017 pkee wahamiaji 6,604  kutoka Guinea waliwasili pwani ya Italia kupitia Libya , na kuifanya Guinea kuwa ni nchi ya pili ukiacha Nigeria yenye Waafrika wengi wahamiaji waliowasili kwa njia ya bahari barani Ulaya.