Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa jinsia kubadili mtazamo wa watu kwa UN

Walinda amani wanawake wakizunugmza na wanawake wanajamii eneo la Ntoto Kivu Kaskazini.(Picha:MONUSCO)

Usawa wa jinsia kubadili mtazamo wa watu kwa UN

Amani na Usalama

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe 8 mwezi huu viongozi waandamizi wanawake kwenye Umoja wa Mataifa wametathmini ushirikishwaji wa mwanamke katika harakati za maendeleo duniani.

Miongoni mwa viongozi hao ni Catherine Pollard, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya menejimenti ambaye amesema msingi wa umuhimu wa kushirikisha wanawake kwenye uongozi bila ubaguzi.

(Sauti ya Catherine Pollard)

“Wanawake kwa sasa ni nusu ya idadi ya watu wote duniani, hivyo hapa UN na katika kazi zake duniani kote. Fikiria ingalikuwaje tusingalikuwa harakati za kusongesha haki za wanawake zisingalikuwa sehemu ya usawa na kile ambacho UN inasimamia.”

 Naye Naibu Katibu Mkuu   wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema hatua ya Umoja wa Mataifa kusimamia kidete haki za mwanamke zinabadili mwelekeo..

(Sauti Amina J Mohammed)

 Bila shaka itahusu uhusiano wa madaraka, na hii itabadili jinsi watu wanafikiria na kufanya kazi na UN.Iwe ni kuanzia kwenye menejimenti au miradi yake au jinsi tunavyohusiana na kile kinachofanyika mashinani.”

 Umoja wa Mataifa nchini ya uongozi wa katibu mkuu Antonio Guterres  umejiwekea  lengo la kufikia asilimia hamsini  ya ajira kati ya wanaume kwa wanawake ndani ya chombo hicho katika ngazi zote.