Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo la ajira kati ya wanawake na wanaume lingali kubwa- ILO

Mamam mchuuzi wa mboga huko Palestina.(Picha:ILO/Tbass Effendi)

Pengo la ajira kati ya wanawake na wanaume lingali kubwa- ILO

Wanawake

Ripoti mpya ya shirila la kazi duniani ILO imesema japo hatua zimepigwa katika harakati za usawa wa kijinsia, bado kuna pengo kubwa kwenye soko la ajira kati ya wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kiwango cha ushiriki wa wanawake duniani kote  katika soko la ajira ni asilimia 48.5 ambacho ni pungufu kwa asilimia 26.5 ikilinganishwa na kiwango cha wanaume kwenye soko la ajira.

Kwa ujumla inamaanisha kwamba katika ajira wanaume wakiwa 10 wanawake ni 6.

Debra Greenflield ambaye ni Naibu Mkurungezi wa ILO kitengo cha sera amesema licha ya kwamba wanawake wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira, usawa

wa mshahara au aina nyingine za ubaguzi bado wanahitaji  kupambana zaidi ili kubadili mwenendo huu usiokubalika katika dunia hii ya leo.

Ripoti hiyo ya ILO imebaini pia kwamba changamoto zingine katika  ukosefu wa ajira  kwa wanawake zinatokana na uwezo kiuchumi wa nchi wanakotoka . 

Imetoa mfano wa nchini nyingi  za Ulaya na Amerika ya Kaskazini ambazo zina uwezo mkubwa kiuchumi zikilinganishwa na nchini za Asia Kusini na Afrika.