Bei ya chakula imepanda kwa aslimia 1.1 Februari :FAO

1 Machi 2018

Ripoti ya Februari ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO imebaini ongezeko la asilimia 1.1 la bei ya nafaka duniani Ikilinganishwa na mwezi Januari mwaka huu.

Kwa mujibu orodha ya viwango vya be iza vyakula ya shirika hilo, ongezeko hilo la nafaka kama ngano, mchele na mahindi limesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya Marekani na  Angentina ambao ni wazalishaji wakubwa wa mahindi duniani.

FAO imesema kutokana na tatizo la ukame katika baadhi ya maeneo ya Amerika kaskazini , Amerika kusini na Kusini mwa Afrika , makadirio ya uzalishi wa unga wa ngano, na wa mahindi mwaka huu yako nchini ya kiwango cha wastani.

Wakati huo, FAO,imesema kwa mujibu wa mavuno ya mazao ya nafaka ya mwaka jana, uzalishaji uliongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka tani milioni 2017 hadi milioni 2642 baada ya marekebisho ya nafaka kutoka Austalia na Afrika magharibi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter