Dola milioni 800 zinatafutwa kusaidia wasyria na wapalestina

30 Januari 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina,  UNRWA limezindua harambee ya kuchangisha fedha  zaidi ya dola millioni 800 kwa wapalestina walioko katika eneo linalokaliwa  la Gaza na ukingo wa magharibi wa mto Jordan. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

UNRWA inasema harambee hii ni ya mpango wa dharura  ambapo dola millioni 400 ni kwa ajili ya wakimbizi wa Syria na zilizobaki kwa ajili ya wapalestina.

Miongoni mwao ni wakimbizi 50,000 wa kipalestina waliotoroka Syria ambao walikimbilia Jordan pamoja na Lebanon.

Akizindua Harambe hiyo mjini Geneva, Uswisi hii leo kamishna mkuu wa UNRWA Pierre Krahenbuhl, amesema idadi ya kubwa ya wapalestina kwenye maeneo yanayokaliwa  na Israel na wale wanaotoka Syria hutegemea mno UNRWA kuwapatia chakula, makazi,  na matibabu.

Amesema kuwa shida ya kifedha ya UNRWA imetokana na Marekani kupunguza mchango wake…

(Sauti ya Pierre Krahenbul)

“Mwaka huu tumejikuta katika njia panda kufuatia uamuzi wa Marekani kupunguza mchango wao wa kifedha. Mwaka jana tulipata dola  millioni 360 kutoka serikali ya Marekani, lakini mwaka huu ilitangaza kutoa millioni 60 tu.”

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter