Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Myanmar wekeni mazingira bora Warohingya warejee: UNHCR

© UNHCR / Andrew McConnell
Watoto waRohingya katika kambi ya Chonkhola huko Chakdhala, Bangladesh.

Myanmar wekeni mazingira bora Warohingya warejee: UNHCR

Amani na Usalama

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR bado kuna mikingamo kuhusu uamuzi wa wakimbizi wa Rohingya kurejea nyumbani kwao Myanmar licha ya serikali za Bangladesh na Myanmar  kukubaliana. Siraj Kalyango na ripoti kamili.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR bado kuna mikingamo kuhusu uamuzi wa wakimbizi wa Rohingya kurejea nyumbani kwao Myanmar licha ya serikali za Bangladesh na Myanmar  kukubaliana. Siraj Kalyango na ripoti kamili.

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Makubaliano ya serikali hizo mbili yanazitaka zihakikishe kuwa wakimbizi hao sio tu wanarejea kwa hiari lakini pia kwa usalama vijijini kwao nchini Myanmar.

Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema hadi sasa  hakuna hakikisho kwa wakimbizi hao kurejea salama na kwa hiari na hivyo kuitolea wito serikali ya Myanmar

(sauti ya Adrian Edwards)

“ Kwa mara nyingine tena tunaitolea wito serikali ya Mynamar iruhusu ufikishaji wa huduma za kibinadamu kwenye  jimbo la Rakhine bila masharti yoyote na pia kuweka hali halisi za kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo”

Aidha amesema kuwa   wakimbizi wengine wanaendelea kuwasili nchini Bangladesh wakitoka jimbo la Rakhine.

Akisisitiza mchakato wa wakimbizi kuweza kuchukua uamuzi wa kurejea kwa hiari ni sharti vigezo kadhaa viwepo akitoa mfano.

(Sauti ya Adrian Edwards)

“ Wakimbizi wanahitaji kufahamishwa kupitia njia muafaka na pia kushauriwa kuhusu hali yenyewe ili kurejea kwao kuweze kuwa salama, kwa hiari na kuwe endelevu.”

Amesema UNHCR iko tayari kuendelea kushirikiana na serikali zote ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo kwa manufaa ya pande zote husika ikiwemo jamii za jimbo la Rakhine.