Mashambulio ya kigaidi bado tishio Mali: Lacroix

23 Januari 2018

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amelihutubia Baraza la Usalama la umoja huo na kuliarifu hali ilivyo hivi sasa nchini Mali, hususan usalama.

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amelihutubia Baraza la Usalama la umoja huo na kuliarifu hali ilivyo hivi sasa nchini Mali, hususan usalama.

Akinukuu ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mada hiyo Bwana Lacroix amesema kuwa inamulika hali kuendelea kuvurugika katikati mwa nchi kukiripotiwa kuwepo kwa mashambulizi  mengi ya kigaidi hususan katika eneo la Mopti.

Ameongeza kuwa serikali ya Mali kwa upande wake inaendeleza juhudi zxake huku Waziri Mkuu aliitisha mkutano wa baraza la mawaziri kujadili hali ya usalama katika eneo la kati.

Kwa upande wake  mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Mali  MINUSMA umeimarisha msaada wake kwa vikosi vya usalama vya  jeshi la Mali  katika jimbo la kati  kufuatia makubaliano na serikali ya Novemba 8.

Aidha amesema MINUSMA inasaidia kupiga jeki pia juhudi za kulinda usalama wa kambi sita  za jeshi la mali kwa gharama ya dolla za kimarekani milioni moja.

Na kwa muda huohuo mashauriano  kuhusu kukamilishwa kwa makubaliano ya kiufundi kati ya G5 Sahel, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya yanaendelea vema na lengo ni kushirikiana pamoja na  mkakati wa pamoja wa kutafuta fedha wa muungano wa Ulaya pamoja na Muungano wa Afrika kabla ya kufanyika mkutano wa wahisani  mjini Brussels, Ubelgiji tarehe 23 mwezi ujao kufuatana na azimio la baraza la usalama nambari 2391.

Aidha Bwana Lacroix ameliambia baraza la usalama kuwa uchaguzi mkuu wa urais ujao nchini Mali ni mwanzo wa sura mpya katika kuleta utengamano nchini humo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter