Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mpakani mwa Syria na Uturuki yatia hofu- OCHA

Watoto wa Syria wanacheza katika kambi ya wakimbizi ya Akcakale, Turkey. Picha: WFP/Berna Cetin (maktaba)

Mapigano mpakani mwa Syria na Uturuki yatia hofu- OCHA

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa juu ya ustawi wa maelfu ya raia wanaokabiliwa na mapigano wakati huu wa operesheni za kijeshi kaskazini-magharibi mwa jimbo la Aleppo nchini Syria.

Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa juu ya ustawi wa maelfu ya raia wanaokabiliwa na mapigano wakati huu wa operesheni za kijeshi kaskazini-magharibi mwa jimbo la Aleppo nchini Syria.

Mapigano hayo yamejikita kwenye wilaya ya Afrin mpakani mwa Syria na Uturuki ambapo ripoti zinaeleza kuwa lengo lake ni kuwang’oa wapiganaji magaidi waliomo nchini Syria.

Katika taarifa yake, ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na misaada ya dharura, OCHA imesema hivi sasa kuna watu zaidi ya 300,000 kwenye eneo hilo wakiwemo watoto, wanawake na wanaume ambapo zaidi ya laki moja kati yao ni wakimbizi wa ndani.

Hofu zaidi ni kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani inaweza kuongezeka kutokana na mapigano na ghasia zinazoendelea.

OCHA imesema hata kabla ya zahma ya sasa, asilimia 60 ya wakazi wa wilaya hiyo ya Afrin walikuwa wanategemea misaada ya kibinadamu.

Kutokana na hali hiyo sasa Umoja wa Mataifa na mashirika wanajiweka sawa ili kuweza kuchukua hatua za haraka za usaidizi kukidhi mahitaji ya raia.