Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani shambulizi la kigaidi mjini Kabul:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Afghanistan. PichaUM/Manuel Elias

Guterres alaani shambulizi la kigaidi mjini Kabul:

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la Jumamosi kwenye hoteli ya Intercontinental mjini Kabul nchini Afghanistan.

Afghanistanshambulii

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la Jumamosi kwenye hoteli ya Intercontinental mjini Kabul nchini Afghanista.

image
Mji wa Kabul nchini Afghanistan. Picha na UNAMA/Fardin Waez
Kufuatia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo kundi la kigaidi la Taliban limedai kuhusika huku akiwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.

Pia Katibu Mkuu ameelezea mshikamano wake na serikali na watu wa Afghanistan katika wakati huu mgumu. Watu wapatao watano wanadaiwa kuuawa na wengine 16 kujeruhiwa huku mamia wakiokolewa wakati wa shambulio hilo.