Sikuchagua muziki bali muziki ulinichagua mimi- mwanamuziki Jermain

11 Agosti 2017

Ni nadra sana kumuona mtu mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino nchini Haiti, kwa kawaida kundi hili linakejeliwa sana. Hiyo ni kauli ya James Germain ambaye ni mwanamuziki mwenye ulemavu wa ngozi kutoka Haiti, anaesema kama mwanamuziki anatumia fursa hiyo kubadili mtazamo potofu wa jamii dhidi ya kundi la watu hao.

Aidha anajikita katika kuchagiza amani nchini mwake hususan kwa kufanya miradi na vijana akishirikiana na wadau ukiwemo Umoja wa Mataifa kwani anaamini ili kubadili jamii ni bora kuwalenga vijana. Basi kwa undani wa makala hii ungana na Grace Kaneiya.