Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi yajeruhi walinda amani na raia Mali-MINUSMA

Mashambulizi yajeruhi walinda amani na raia Mali-MINUSMA

Mapema leo asubuhi, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, umeripoti kuwepo mashambulio ya kigaidi yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya kwa askari walinda amani wawili na na raia mmoja.

Kwa mujibu wa MINUSMA, shambulio la kwanza limetokea jimboni Kidal baada ya gari kushambuliwa na kilipuzi Kaskazini mwa taifa hilo. Gari lililoshambuliwa limeharibiwa vibaya.

Ujumbe huo umeongeza kuwa kulikuwa na shambulio jingine la kigaidi ambapo watu wasiofahamika waliojihami kwa silaha walishambulia wakilenga kambi za vikosi vya kitaifa vya Mali, katika eneo litwalo Timbuktu.

Akizungumzia mashambulizi hayo, hususani lile la Timbuktu, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, amewaambia waandishi wa habari mjini New York Marekani kuwa.

(Sauti ya Dujarric)

‘‘MINUSCA walituma helkopta yake ya kushambulia katika eneo hilo ili kusaidia vikosi vya Mali nakuwezesha kuwaokoa majeruhi kwa kuwachukua kwa njia ya anga.’’

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa MINUSMA Mahamat Saleh Annadif, amelaani vikali shambulio hilo na kuelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa hali ya uslama kaskazini na kati mwa Mali.