Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto zaidi ya 60 wauawa kwenye shambulio la basi Aleppo-UNICEF

Watoto zaidi ya 60 wauawa kwenye shambulio la basi Aleppo-UNICEF

Baada ya miaka sita ya vita na madhila ya kila aina Syria yaliyovunja mioyo ya familia nyingi, jinamizi lingine laibuka. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake watoto zaidi ya 60 wamearifiwa kuuawa katika shambulio kwenye msafara wa basi nje kidogo ya mji wa Aleppo mwishoni mwa wiki.

Msafara huo ulikuwa umebeba familia ambazo tayari zimeteseka mwa muda mrefu na sasa walionusurika wanalazimika kubeba tena mzigo wa machungu ya kuondokewa na wapendwa wao.

Bwana Lake amesema la kujifunza katika shambulio hilo sio tu hasira bali kuwa na nguvu mpya ya kuhakikisha wanafikiwa maelfu ya watoto wasio na hatia kote Syria na wanapatiwa msaada na faraja. Pia kuhakikisha matumaini ya Wasyria ya kukomesha vita hivyo yanatimia