Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanorejea makwao Nigeria wakabiliwa na changamoto: UNHCR

Wanorejea makwao Nigeria wakabiliwa na changamoto: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema changamoto za kibinadamu zinaendelea kuibuka nchini Nigeria wakati huu ambapo serikali ya nchi hiyo inaendelea kufungua maeneo zaidi na kuwezesha kurejea kwa maelfu ya watu kutoka maeneo yalikuwa yanakiliwa na kundi la kigaidi, Boko Haram.

UNHCR inasema kiwango cha uharibifu kinatajwa kuongezeka sanjari na changamoto hizo Kaskazini Mashariki ambapo hadi sasa maelfu ya watu kutoka jimboni Maiduguri wamehamishiwa katika miji ya Dikwa, Kodnuga na Mafa.

Changamoto nyingi zinawakabili wanaorejea mathalani katika mji uitwao Gwoza uliopo kilometa 150 kutoka Maiduguri, limebaini shirika hilo baada ya kuzuru katika mji huo.

Takribani watu 300,000 walikimbilia Maidurguri mwaka jana na mwaka huu wakihepa utawala na mapigano mfululizo ya miezi minane wa Boko Haram.