Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati El Nino ikiaga Ethiopia La Nina inanyemelea:FAO

Wakati El Nino ikiaga Ethiopia La Nina inanyemelea:FAO

Ethiopia sasa inautupa mkono msimu mbaya wa Elnino kuwahi kutokea katika nchi hiyo, lakini uwezekano wa msimu mkubwa wa La nina unanyemelea limesema shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Shirika hilo linatoa ombi la dola milioni 45 ili kusaidia sekta ya kilimo ya Ethiopia kuendelea na uzalishaji.

Wito huu mpya wa msaada umetokana na tathimini ya hali ya kibinadamu nchini humo iliyotolewa leo.

Ili kufafanua zaidi kuhusu hali hiyo huyu hapa Pierre Vauthier kiongozi wa kitengo cha kukabiliana na madhila cha FAO nchini Ethiopia.

(SAUTI YA PIERRE VAUTHIER)

 “La Nina itakuja kati ya Oktoba Novemba, na Mashariki mwa Ethiopia kwenye muinuko kutakuwa na mafuriko yatakayoharibu vitu vingi ikiwemo majengo , labda barabara na pia yataathiri kilimo na mifugo, na mabondeni kutakuwa na ukame wa hali yajuu hali itakuwa mbaya sana”