Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaume na wanawake walio wengi wanapinga ukeketaji:UNICEF

Wanaume na wanawake walio wengi wanapinga ukeketaji:UNICEF

Takribani theluthi mbili ya wanaume, wanawake, wavulana na wasichana katika nchi ambako ukeketaji unafanyika wansema wanataka vitendo hivyo vikome kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Katika nchi ambako takwimu zimekusanywa , asilimia 67 ya wasichana na wanawake, na asilimi 63 ya wanaume na wavulana wanapinga vitendo vya ukeketaji katika jamii zao.

Kwa mujibu wa Francesca Moneti, afisa wa UNICEF na mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto, ingawa ukeketaji unahusishwa na ubaguzi wa kijinsia utafiti wa UNICEF umebaini kwamba idadi kuwa ya wanaume na wavuka hawapendo lakini kwa bahati mbaya nia ya kutaka kutokomeza ukeketaji haiwekwi bayana na kuna wanawake na wanaume ambao bado wanaamini kwamba ukeketaji unahitajika ili waweze kukubalika katika jamii.

Pia utafiti umebaini nchi kama Guinea ambayo ina kiwango kikubwa cha ukeketaji wanaume asilimia 38 wanaupinga wakati wanawake na wasichana wanaopinga ni asilimia 21.

Pia asilimia 46 ya wanaume na wavulana nchini humo wanaona hauna faida ikilinganishwa na asilimia 10 tu ya wasichana na wanawake wanaoamini hivyo.