Skip to main content

Ban ziarani Cuba kushuhudia makubaliano ya kusitisha mapigano Colombia

Ban ziarani Cuba kushuhudia makubaliano ya kusitisha mapigano Colombia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, yupo ziarani nchini Cuba, ambako anatarajiwa kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuweka chini silaha baina ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC, na hivyo kumaliza mzozo uliodumu muda mrefu zaidi barani Amerika ya Kusini.

Awali, makubaliano hayo yalikuwa yamepangwa kutiwa saini mnamo tarehe 23 Machi mwaka huu wa 2016, lakini pande kinzani hazikuweza kukubaliana kuhusu masuala muhimu.

Hafla hiyo ya kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano itahudhuriwa pia na marais wa Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.