Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wafanyakazi wa umma ni muhimu katika utekelezaji wa SDG's:Ban

Mchango wa wafanyakazi wa umma ni muhimu katika utekelezaji wa SDG's:Ban

Katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma hii leo Juni 23, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mchango wao unatambulika na kwa kuboresha maisha ya watu.

Amesema juhudi zinazofanywa na wanawake na wanaume katika kutoa huduma kwa umma ni muhimu sana kwa ajili ya utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s.

Kwa mujibu wa Ban kila lengo lina uhusiano na utoaji huduma kwa umma kuanzia afya hadi elimu, usalama hadi utawala wa sheria, maji, nishati hadi sera za uchumi na zaidi.

Ameongeza kuwa nchi zote watu wanahitaji huduma ya umma ambayo ni bora, inayojitosheleza na iliyosheheni, ambayo inazingatia maadili na kujumuisha wote na inapaswa kujikita katika kuhudumia na kuboresha maisha ya watu masikini na wasio jiweza.