Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

John Ashe afariki dunia

John Ashe afariki dunia

John Ashe, ambaye alikuwa rais wa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amefariki dunia. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats..

Mwendazake John Ashe! Hapa akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha kukabidhi madaraka kwa Rais aliyefuatia baada ya yeye kuhudumu kwa kipindi cha mwaka 2013/2014!

John William Ashe amefariki dunia siku ya Jumatano.

Kufuatia kifo hicho, Rais wa sasa wa Baraza Kuu, Mogens Lykketoft ametuma salamu za rambirambi kwa mjane, marafiki na kwa wale wote waliowahi kufanya kazi na Ashe ambapo aliwahi pia kuwa mwakilishi wa Antigua na Barbuda.

Tangu mwezi Oktoba mwaka 2015, Ashe amekuwa akikabiliwa na tuhuma za uhalifu nchini Marekani zikihusiana na kipindi chake cha uongozi wa Baraza Kuu.

Bwana Lykettoft amesema licha ya tuhuma hizo ambazo bado hazijathibitishwa, Ashe kwa miaka mingi amekuwa mwanadiplomasia anayejituma na maarufu New York, na ndani ya Umoja wa Mataifa.

Amesema anatambua kifo chake kitaleta masikitiko miongoni mwa aliofanya nao kazi.