Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya dharura ya WHO kukutana kujadili Zika

Kamati ya dharura ya WHO kukutana kujadili Zika

Shirika la afya ulimwenguni, limeitisha kikao cha tatu cha kamati yake ya dharura kuangalia mwelekeo ugonjwa wa Zika na ripoti za ongezeko la athari za mishipa na neva na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo.

Taarifa ya WHO imesema kamati hiyo itakayokutana kesho huko Geneva, Uswisi, itaangalia iwapo virusi vya Zika bado ni tishio kwa afya ya umma duniani na kupitia mapendekezo ya awali ya kamati hiyo ya udhibiti na iwapo iwapo hatua mpya zinahitajika.

Wanakamati pia watapitia taarifa kutoka kwa wataalamu na watafiti juu ya hatari ya kuenea kwa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu, hususan kwa wasafiri wa kimataifa na mikusanyiko wakizingatia zaidi michezo ya olimpiki ya Rio.

Mathalani watapatiwa taarifa mpya kutoka Brazil juu ya hali ya Zika hivi sasa na mwelekeo wa kuenea kwa maambukizi na hatua zinazochukuliwa kudhibiti vimelea vya mbu Aedes ili kulinda wananchi na wasafiri.