Neno la wiki- Mazishi au maziko?

29 Aprili 2016

Ijumaa ya tarehe 29 Mei mwaka 2016 tuliangazia matumizi ya maneno maziko na mazishi. Mtaalamu wetu alikuwa Onni Sigalla, mhariri mwandamizi,  Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Bwana Sigalla, mazishi huanza pale mtu anapokata roho au kufariki dunia, shughuli zote kama zile watu kukusanyika na kupeana taarifa mbali mbali ikiwemo kuchangishana, hayo ni mazishi na hayapangiwi muda.

Lakini maziko ni kitendo cha kuhifadhi mwili wa marehemu kaburini na kitendo hiki ndiyo huweza kupangiwa muda. Mathalani utasema maziko yatafanyika saa kumi jioni lakini mazishi yanaendelea nyumbani kwa marehemu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter