Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya kupitia Intaneti zaleta mabadiliko Ulaya

Huduma za afya kupitia Intaneti zaleta mabadiliko Ulaya

Huduma za afya kupitia mtandao wa intaneti zinaleta mafanikio makubwa kwenye nchi nyingi za Ulaya, imebaini ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO).

Taarifa iliyotolewa leo imeeleza kwamba teknolojia za digitali zimesababisha mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za afya kupitia rikodi za afya za kielektroniki, utoaji huduma ya afya kwa njia ya mtandao, matumizi ya mitandao kwa ajili ya kujifunza kuhusu afya, na kadhalika.

Kwa mujibu wa WHO, mabadiliko hayo yamechangia kuwezesha zaidi watumizi wa huduma za afya, kuokoa maisha na kupunguza matumizi ya fedha.

Hata hivyo, ripoti imeonyesha kwamba udhibiti wa kisheria unahitajika katika usambazaji wa teknolojia hizo, hasa kwa ajili ya kuzuia matumizi ya kibiashara ya takwimu na data hizo.