Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari Ufilipino

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi wa habari Ufilipino

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari kutoka Ufilipino, Elvis Ordaniza, ambaye ameuawa tarehe 16 Februari kwenye eneo la Mindanao, Ufilipino, kwa kupigwa risasi.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo na UNESCO Bi Bokova ameomba uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji hayo.

Ameongeza kwamba waandishi wa habari wanapaswa kuwa na haki ya kufanya kazi zao kwa usalama, akizisihi mamlaka za serikali kufanya lolote liwezekanalo ili kupeleka watekelezaji wa uhalifu huo mbele ya sheria.