Skip to main content

Idadi ya wahanga wa mashambulizi Afghanistan yafikia rikodi mpya

Idadi ya wahanga wa mashambulizi Afghanistan yafikia rikodi mpya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umesema kwamba idadi ya wahanga wa machafuko nchini humo kwa mwaka 2015 imeweka rekodi mpya ya kihistoria.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNAMA iliyotolewa leo kwa ushirikiano na Ofisi ya Haki za binadamu, watu zaidi ya 3,500 wameuawa mwaka 2015, huku wengine wapatao 7,500 wakijeruhiwa.

Idahi hiyo ni ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo mkuu wa UNAMA Nicholas Haysom amesema uhalifu huo haukubaliki, akitaka watu kuwafikiria watoto walioachwa na ulemavu au waliopoteza wazazi wao katika mashambulizi hayo.

Ripoti inaonyesha pia kwamba mashambulizi dhidi ya wanawake yameongezeka kwa asilimia 37.

Waasi wanaopinga serikali ya Afghanistan wanadaiwa kuwa wametekeleza asilimia 60 ya uhalifu ulioripotiwa.