Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi walaaniwa na Katibu Mkuu

Mpango wa ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi walaaniwa na Katibu Mkuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu ripoti zinazoonyesha kwamba serikali ya Israel imeidhinisha kutangazwa kwa eka 370 kuwa ardhi ya taifa, kwenye ukingo wa Magharibi, kusini mwa Jericho.

Amesema, uamuzi huo ukitekelezwa, utakuwa kitendo cha kujitwalia eneo la ardhi kubwa zaidi tangu Agosti mwaka 2014.

Katibu Mkuu amekariri wito wake kwa Israel akiitaka ibadili sera ili kuimarisha maisha ya wapalestina. Ameongeza kwamba vitendo vya kujitwalia ardhi ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa na vinaenda kinyume na maazimio ya serikali ya Israel ya kuiunga mkono suluhu ya mataifa mawili ili kutatua mzozo huo.