Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yatosha sasa vita Syria: UM

Yatosha sasa vita Syria: UM

Zaidi ya mashirika 120 ya misaada ya kibinadamu  na Umoaj wa Mataifa yametoa tamko la pamoja la kuitaka dunia kuungana na kukomesha vita nchini Syria.

Machafuko nchinibumo yameingia mwaka wa sita sasa zaidi yaw tau 200,000 wamefariki dunia, huku wengine zaidi milioni 13 ndani na nje ya nchi wakiwa wanahitaji misaada.

Miongoni mwa mashirika yaliyotoa tamko hilo ni lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambapo afisa wake John Budd amezungumza na radio ya Umoja wa Mataifa

(SAUTI BUDD)

‘Nafikiri ni vyema kuhamasisha watu kuwafahamisha hali ilivyo. Kukumbusha dunia kwamba ufikishwaji wa misaada, masula ya kibinadamu na watu wenyewe wasisahaulike.’’