Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafi ni msingi katika kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Dadaab: mtalaam wa UNHCR

Usafi ni msingi katika kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Dadaab: mtalaam wa UNHCR

Nchini Kenya, zaidi ya watu 1,000 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab, watu 10 wakiwa wamefariki dunia.

Kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR linajitahidi kuimarisha kiwango cha usafi na kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa idhaa hii, mtaalam wa UNHCR kuhusu maji safi na kujisafi Osman Yussuf Ahmed ameeleza kwamba kiwango cha upatikanaji wa maji kambini ni kizuri kikiwa ni lita 24 kwa mtu kila siku, na huduma za vyoo zikipatikana kwa asilimia 56 ya familia zilizoko kambini.

Hata hivyo, amesema kwamba UNHCR inahaha kuhakikisha kiwango cha usafi kinaimarishwa na vyanzo vya maambukizi vinadhibitiwa.

Hapa ameanza kwa kufafanua idadi ya wagonjwa wa kipindupindu.